Tuesday, December 30, 2014

Why Tanzanian graduates fail to impress in job interviews

Why Tanzanian graduates fail to impress in job interviews



Head of Human Resources Unit with World Food Programme, Tanzania Jamila Isdory

The current economic situation creates a sense of urgency in devising ways to boost the creation of jobs, and to improve young people’s access to those jobs. 
 
One distinct aspect of the current global labour market is that relatively high unemployment coexists with widespread recruitment challenges faced by employers.  
 
In other words, while there is currently excess labour supply in the aggregate, the distinct labour markets for specific skill sets are highly segmented and many employers are having difficulty finding individuals with the right skill sets for the business tasks at hand.  
 
It is not a secret that there is a widespread perception, right or wrong, that some Tanzanian graduates are being deliberately passed in favour of foreigners when it comes to job placements. 
 
Speaking to this paper in an exclusive interview over the weekend in Dar es Salaam, Head of Human Resources Unit with World Food Programme, Tanzania Jamila Isdory said that there are a lot of reasons that cause many Tanzanian job seekers fail in interviews.
 
Having worked in the human resources unit with different UN Agencies working in Tanzania mentioned the first reason that make many interviewees perform badly in interviews as lack of preparation.
 
To her preparation is key to having a great interview. “As a candidate you need to invest time in knowing the company and the job you are interviewing for.”
 
She further said that an interviewee should know what are the main objectives of the companies, how do they operate, where do they operate, what are the core functions for post and how does the job contribute to the company’s objectives? 
 
“By understanding these aspects, you can start preparing examples and evidences on how your skills, education, work experience, and the like are a perfect fit for the job. This will also help you to identify what you are bringing to the table and present your work more clearly and confidently,” she explained.
 
She says if job seekers will not be able to link their education, skills and experiences to the job they are applying for “it is not enough to say I have an MBA or I have five years of experience; instead you need to clarify how the MBA and the five years of experience will benefit the post and company in general.”
 
 “Failing to sell yourself – Understandably this is tricky since it is very hard to talk about yourself, but in interviews you need to put your modesty aside, many candidates make the mistake of assuming that the hiring managers have read their CVs in details, so they know their skills and potentials.”
 
She adds that hiring managers receive more than 100 applications for each post; they spend a few minutes in each CV.
Isdory says candidates need to step out of their comfort zone and use their strong points to their advantage. If you designed a new process that helped to simplify work load or wrote a proposal that won a grant, or set up a filling system that improved record keeping use it to make your case.
 
She notes that some job seekers fail to impress in job interviews because they are not solution oriented. That means they are not problem solving, but they are part of the problem.
 
She says according to her experience, when a company advertises a vacancy, one should know that it has a problem that needs to be resolved. It can be expansion of business, introduction of new services or clearing some work backlog.
 
At times this information is indicated in the advert that “We are hiring for an X position to help with implementation of this project.”
 
Isdory says “When preparing for the interview, you need to think how you can be the solution to the challenge faced by the company and come up with a few suggestions or ideas to present in the interview.”
 
Bad attitude/manner is another factor that causes job seekers to perform poorly in their interviews.
She says interviewees should avoid any bad attitudes when they are invited for an interview. 
 
According to Isdory some of these bad attitudes are such as for an interviewee to show up being late for an interview, chewing gum during the interview, keeping his cell phone on and speaking badly about previous employer. She says that is not the way to win in interviews, but it can rather deny him that post.
 
Asking wrong questions: 
She urges prospective candidates to ask work related questions, when they are given that opportunity instead of asking silly questions.
 
“This is not the time to ask about maternity leave, Hiring Managers want someone who can work on a continuous basis, since interviews are costly and time consuming; no one will hire you if they know you are thinking of taking leave soon,” she urges.
 
So in order to reach the over 800,000 Tanzanian graduates who complete their high education every year to easily secure jobs meant for them Isdory has created a website that offers free information to help job seekers, such as CV writing, and preparation for interviews; known as ww.interviewcoachtz.com

Ukiukwaji wa haki za binadamu na unyama ukatili ulipitiliza wa serikali ya ccm










2014 ni mwaka ambao ulijaa mauaji mengi ya watu wasio na hatia.
Idara ya polisi ndio inayoongza kwa kupiga na kuua watu bila sababu na polisi wamefanya hivyo kwa maagizo ya ccm.na polisi bila wao kujua wamejenga uadui mkubwa na wananchi na hii hatari kwao.
Kuna mapigano ya wakulima na wafugaji nchi nzima haya Nayo yamesababisha mauaji ya watu wengi hadi watoto.
Haya yote ukiyachunguza vizuri utakuta chama kinachoongoza nchi kimeshindwa kwa sehemu kubwa sana kusimamia 
sheria za nchi na kuongoza.
Rushwa imetawala kila kona ya nchi hadi mahakaamani ni rushwa ukweli ni kwamba ccm imeshindwa kuongoza nchi.
Watanzania lazima tuamke tutafute chama mbadala ili kuiondoa serikali ya ccm na kuweka chama kingine madarakani.

Picha juu zina onesha baadhi tu ya matuki yaliojaa umyama na ukiukwaji wa haki za binadamu ukatili wa jeshi la polisi kwa binadamu mauaji ya raia wasio na hatia mauaji ya waandishi wa habari kiukweli ni unyanyasaji uliopilizia na ukiukwaji wa haki na uhuru wa binadamu,
Matumizimabovu ya madaraka yanapelekea mauwaji na kunyanyaswaji wa rai kimsingi yote haya yanasababishwa na uroho wa madara wa serikali ya CCM
TUTAFAKARI WATANZANIA JE TUENDELEE CHINI YA SERIKALI YA CCM AU TUIONDOE HIO SERIKALI?
?

Serikali ya pata kigugumizi kusaini mkataba wa demokrasia(ACD)

Serikali inangoja nini kusaini Mkataba wa Demokrasia Afrika?




























waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro.

Serikali inahojiwa ni kipi kinachoizuia kukukubali kusaini mkataba wa Demokrasia Barani Afrika (ACD)? Pamoja na hayo inahimizwa  na  wadau wa maendeleo na utawala bora kusaini  ili kukuza kiwango cha demokrasia, uwajibikaji, utawala bora na uwazi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (Jukata), Deus Kibamba, anasema katika mahojiano maalumu mapema wiki hii Jijini Dar es Salaam kuwa, Tanzania ni mojwapo ya nchi zinazounda  Umoja wa Afrika (AU) ambayo haijasaini mkataba huo tangu mwaka 2007.

Kutosainiwa kwa mkataba huo, anasema husababisha taifa kuendeshwa na watendaji wasiozingatia sheria, utawala bora, haki za binadamu na za walemavu, uhuru wa taarifa,  kukosekana kwa uwazi  na wajibikaji hasa nyakati za  uchaguzi.

“Tunashuhudia ongezeko la vitendo vya ufisadi vinavyoliabisha taifa hadi ngazi ya kimataifa,  baadhi ya viongozi kutumia udhaifu wa kutosainiwa kwa azimio la ACD la mwaka 2007, hivi kuna tatizo gani kutosaini?,”anahoji Kibamba .

Kwa muktadha huo, anasema serikali inatakiwa kujitathimini kupitia sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji  mwaka huu, kashfa za wizi wa fedha zilizokuwa kwenye akauti ya madeni ya nje (EPA) na tuhuma za  Richmond ili kwayo iwe funzo na msukumo wa  kuona umuhimu wa kusaini mkataba huo katika mkutano ujao wa AU.

Anasema kusimamishwa , kufutwa kazi na kuonywa kwa baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri hapa nchini ni matokeo ya ukosefu wa utendaji usiokuwa makini kutokana na kukosekana kwa shinikizo la kisheria kama vile mkataba unaotaka utiifu katika masuala mtambuka kama vile uchaguzi.

Mkataba huo pamoja na mambo mengine unazitaka nchi wanachama wa AU kuzingatia haki, uwazi, kupambana na vyanzo na viashiria vya migogoro inayoweza kutokana na uchaguzi, kuboresha taasisi zinazohamaisha uchaguzi na demokrasia.

Pia uchaguzi huru na wa haki katika nchi wanachama,uhuru wa kisheria, utawala wa kiutendaji unaochochea kukua kwa demokrasia na utawala bora pamoja na  uwazi kulingana na azimio na kanuni za AU.

Unapofika wakati wa uchaguzi, mkataba huo unaonya nchi wanachama kutoruhusu jeshi kuingilia shughuli za uchaguzi, kuwepo kwa uwazi na upatikanaji wa taarifa za uchaguzi kwa wakati ikiwamo matokeo yaliyotokana na upigaji kura.

Mambo mengine ni  kutokuwepo kwa  vitendo vya kihuni ambavyo mkataba huo unavitafsiri  kuwa ni pamoja na uchakachuaji wa kura, kuharibu uchaguzi kwa makusudi kwa masilahi ya mtu au chama chochote cha siasa na mambo mengine yanayoendana na hayo.

Kadhalka nchi wanachama wanatakiwa unapofika wakati wa uchaguzi kutambua thamani ya haki za binadamu kama vile walemavu, haki za wanawake,makundi yasiyotambulika na maalumu, kuhamasisha utawala bora na haki.

Kibamba ammbaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Taarifa kwa Umma (TCIB) anaona kama  Tanzania haijaweza kupelekea bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ya habari licha ya viongozi waandamizi kauhidi mara kwa mara kat ika mikutano ya ndani na nje ya nchi.

Anasema kwa nyakati tofauti Rais Jakaya Kikwete akiwa nchini Uingereza na Marekani, aliahidi kufikishwa bungeni kwa muswada wa habari kabala ya kumaliza kipindi chake cha uongozi, kauli ambayo amewahi kuirudia akiwa  hapa nchini pia.

“Ninaamini kwamba kupata, muswada wa habari kabla ya kumaliza muda wake mwaka 2015  ni kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano…mimi mwenyewe hivi karibuni nimeshawahi kumuuliza Spika wa Bunge Anne Makinda ikiwa huenda bunge lijalo mwezi Februari, 2015 au kabla ya Bunge la Bajeti 2015/2016 ana mpango wa kupokea muswada wa habari, lakini amenihakikishia kwamba katika orodha yake hakuna kituo kama hicho,”alidai.

Wakati Tanzania ikiendelea kusuasua kupeleka bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya  Vyombo vya Habari, Kenya wamepitisha Sheria mpya ya Usalama inayovibana vyombo hivyo na kuzua utata mkubwa na ikiwa ni pamoja na wabunge kuchapana makonde ndani ya mkutano  wa bunge.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni bunge nchini humo liligeuka `uwanja wa vita’ kutokana na baadhi ya wabunge kunyukana makonde, kuchaniana nguo na kurushiana matusi, maneno ya kebehi na kukashifiana baada ya kugawanyika kuhusu muswada huo ambao ulipitishwa kwa nguvu.

Tayari muswada huo umesainiwa na Rais Uhuru Kenyatta na sasa ni  sheria mpya ya usalama. Serikali ya Marekani  imeonyesha kutoridhishwa na namna Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usalama ulivyopitishwa nchini humo.

Kwa upande wa Tanzania imekuwa vigumu kuwa na sheria ama kanuni zinazotekelezeka za kuwabana viongozi wasiowaadilifu kwa kuwa hata ndani ya katiba pendekezwa masuala ya uadalifu kuwa tunu ya taifa yalipingwa hadharani. Hata hivyo sheria ya maadili na utumishi wa umma ni kiini macho kwa kuwa hakuna kinachoweza kumbana au kumuwajibisha kiongozi wa umma anayekiuka maadili ya utumishi.

Kiporo cha prof. Muhongo chakaribiakuchacha

Muhongo siku zahesabika wizara ya nishati na madini


Shinikizo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, limezidi kushika kasi baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), kumuomba Rais Jakaya Kikwete, kumwajibisha ili kupisha nafasi hiyo ichukuliwe na mtumishi mwenye sifa ya kuutumikia umma.

Desemba 22, mwaka huu, Rais Kikwete alisema katika hotuba yake kwa taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kwamba amemuweka kiporo Profesa Muhongo kwa siku mbili hadi tatu kwa kuwa uchunguzi dhidi yake ulikuwa unaendelea.

Hata hivyo, tangu wakati huo, zimeshapita takriban siku tisa bila Rais Kikwete kutangaza hatima ya Profesa Muhongo kama anatimuliwa ama kubaki katika nafasi yake.

Jukata wanamuomba Rais Kikwete kuchukua hatua hiyo kutokana na Profesa Muhongo kuhusishwa katika kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Limesema hatua hiyo inapaswa kuchukuliwa na Rais Kikwete haraka dhidi ya waziri huyo kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali ya nchi kwa sasa.

Masuala hayo yanayohusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu akaunti hiyo kutokana na taarifa zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mengine yanahusu zoezi la uandikishaji wa Watanzania katika daftari la kudumu la wapigakura katika mfumo mpya wa BVR, uandikishaji wa vitambulisho vya taifa, ambayo alisisitiza yakamilike kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

Mwakagenda alisema iwapo Rais Kikwete anaona utendaji wa Profesa Muhongo unafaa, ampe kazi binafsi ya kusimamia mashamba na siyo kuutumikia umma wa Watanzania.

Hatua ya Jukata ya kutaka Profes. Muhongo kuondolewa katika wadhifa huo kwa hoja kwamba hana tena sifa za kushika nafasi hiyo ya utumishi wa umma, ni mwendelezo wa mashinikizo yanayotolewa na makundi kadhaa ya jamii kufuatia maazimio ya Bunge ya mikutano ya 16 na 17 lililoahirishwa Novemba 29, mwaka huu.

Mbali na Rais Kikwete kumfukuza kazi Profea Tibaijuka, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ameshamsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake za kuhusika na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.

Alimshauri Rais Kikwete kujipa muda wa kusikiliza ushauri wa wataalam walioko nje ya serikali, ambao watamuonyesha nia ya kutaka kunyoosha maadili ya uongozi wa kisiasa na utumishi wa umma.

“Kwa hivi sasa, wasaidizi wake wanashindwa kumshauri Rais kwa kuogopa kubanwa wao wenyewe, hivyo wameweka wigo na kuzuia ushauri huru kumfikia Rais. Na hii ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu,” alisema Mwakagenda.

Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, Mwakagenda alisema Katiba inayopendekezwa haina uhalali wala sifa.

Alisema katiba hiyo imependekezwa kwa ajili ya viongozi wachache, kwani kimeondolewa kipengele cha wananchi kuwadhibiti viongozi.

Aliongeza kuwa katiba hiyo pia ilipitishwa bila ya kuwapo kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kukosekana kwa theluthi mbili kutoka Zanzibar.

“Bunge la Katiba halikufanya vizuri na kulitokea mgawanyiko. Maridhiano hayakuwapo. Katiba hii ni mbaya. Ni ya viongozi. Haimfai mwananchi,” alisema Mwakagenda.

Kutokana na hali hiyo, alipendekeza kuahirishwa upigaji kura ya maoni ya Katiba mpya uliopangwa kufanyika Aprili, mwakani.

Badala yake, alishauri kuitishwa mkutano mkuu wa taifa kuhusu Katiba utakaoshirikisha wadau na vyama vya siasa na kutoa mwongozo wa masuala yenye utata.

“Mchakato usimamishwe, Rais ajaye ataundeleza, tayari Rais Kikwete ameshajijengea sifa na heshima kwa kuuanzisha mchakato huu. Pia Watanzania wengi hawajafahamu kilichopendekezwa, kwani bado hawajapata nakala ya Katiba na Wizara ya Katiba na Sheria imeshasema haijachapisha nakala,” alisema Mwakagenda.

MNYIKA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitawahamasisha wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuibana serikali bungeni kulieleza Bunge sababu za kushindwa kuwafungulia mashitaka ‘wapambe’ wa watu wanaotuhumiwa kuiba nyaraka za Bunge.

Nyaraka za Bunge zilizoibwa ni zile zinazohusu ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu miamala, iliyofanyika katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Tukio hilo lilitangazwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma Novemba 23, mwaka huu, ambalo katika taarifa yake, lilisema kuwa limewatia mbaroni vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za ofisi ya Katibu wa Bunge isivyo halali.

Mbali na kuiba nyaraka hizo, vijana hao wanadaiwa kuzichakachua na kisha kusambaza mitaani ripoti ‘feki’ ya CAG.

Kauli hiyo ya Chadema ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Tanzania Bara), John Mnyika, wakati akihutubia mkutano wa hadhara juzi jioni, katika eneo la Pasua Sokoni, Manispaa ya Moshi.

Alisema kwa kuwa mamlaka ya uteuzi haijafanya uamuzi kwa ukamilifu kuhusu maazimo manane ya Bunge, Chadema itawahamasisha wabunge hao kuishinikiza serikali kueleza kwa nini inachelea kuwafikisha mahakamani wanaodaiwa kuiba nyaraka hizo.

Mnyika alisema hadi kufikia Januri 27, mwakani, kama serikali itakuwa haijawafungulia mashitaka walioiba nyaraka hizo na kuzisambaza mitaani kinyume cha sheria, atawahamasisha wabunge kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutoa maelezo inakuwaje inawalinda hadi sasa watuhumiwa hao.

“Wangapi mko tayari kupiga kura na kusimama upande wa haki? Wanyooshe vidole. Bunge linalokuja tutawahamasisha wabunge wa pande zote kuhoji ni kwa nini serikali inachelea kuwafikisha mahakamani wale walioiba nyaraka za ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha hizi,” alisema Mnyika.

Awali, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa na Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffari Michael, alimweleza Mnyika kwamba manispaa hiyo itaunda mabaraza ya maendeleo ya kata 11 kutokana na kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji.

“Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, sisi tuko vizuri katika agizo la Rais Jakaya Kikwete, kuhusu ujenzi wa maabara. Hadi sasa Manispaa ya Moshi tumefanikiwa kukamilisha maabara 40 kati ya 49,” alisema Michael.

Aliongeza: “Hii ni hatua kubwa na ambayo wenzetu wanajiuliza, inakuwaje wapinzani wanafanikiwa kuliko maeneo yanayoongozwa na chama tawala.”

Akihutubia mikutano ya hadhara iliyofanyika Shule ya Msingi Chombo kata ya Uru Kusini na Kirima Kati, Jimbo la Moshi Vijijini, Mnyika aliwataka viongozi wa Chadema kuanza operesheni maalum ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura kwa kuwa vitambulisho walivyonavyo havitatumika katika kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa pamoja na uchaguzi mkuu.

“Lazima muwaambie ukweli wananchi wa majimbo ya Siha, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Same Mashariki, Same Magharibi, Mwanga na Hai wajitokeze, wasiache kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura, kwa sababu vitambulisho walivyonavyo havitatumika katika kura ya maoni wala uchaguzi mkuu ujao,” alisema Mnyika.

Mvua za jana zaonyesha udhaifu wa miundombinu dar

Mvua yaleta maafa










Mvua  zilizonyesha jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini jana, zilisababisha maafa na kizazaa kikubwa kwa wakazi huku miundombinu mbalimbali hususan ya barabara katika mitaa mbalimbali ikifinikwa maji.

Jijini Dar es Salaam, mvua hizo zilianza saa 4:30 asubuhi na kunyesha kwa nguvu kwa takriban saa mbili, hali iliyosababisha barabara katika mitaa mbalimbali ikiwamo ya Posta na maeneo ya katikati ya jiji hilo kufurika maji na kufanya magari kupita kwa shida.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa maeneo mengi katika ya Jiji na mabondeni, yalifurika maji na kusababisha magari mengi na pikipiki kupita kwa shida huku na waenda kwa miguu nao wakitembea kwa taabu.

Aidha, hali hiyo ilisababisha foleni kubwa za magari katika baadhi ya mitaa hasa katikati ya Jiji.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za vifo katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na mvua hizo licha ya kuwapo kwa usumbufu mkubwa kwa wakazi wake.


MUME, MKE WAFA WAKIWA BARAZANI

Wakati hayo yakitokea jijini Dar es Salaam, mkoani Tabora watu wawili, mke na mume, wakazi wa kijiji cha Lughubu kata ya Itumba wilayani Igunga, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11:00 jioni wakiwa wamekaa barazani kwenye nyumba wanayoimiliki wanandoa hao, Ernest Makala (90) na mkewe Pelepetua Petro (80).

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mmoja wa watoto wa marehemu, Anastazia Ernest, alisema wazazi wake walikuwa wamejipumzisha nyumbani kwao, lakini  ghafla ukuta wa nyumba ulibomoka na kuwaangukia walipokuwa wamekaa.

“Ni kweli sisi watoto tumepata pigo kubwa kwani wazazi wetu wawili wamefariki dunia, mimi nilipigiwa simu na majirani wakiniambia wazazi wangu wamepondwa na ukuta wa nyumba. Nilipofika katika eneo la tukio, nilikuta baba amefariki dunia," alisema Anastazia huku akibubujikwa na machozi.

Mtendaji wa kijiji  cha Lughubu, Hussein Mohamed, alisema yeye baada ya kufika eneo hilo, alikuta wananchi wakiwa tayari wametoa kifusi cha udongo wa nyumba iliyoanguka huku mume, Ernest Makala, akiwa tayari amekwisha kufariki dunia.

“Mimi nilikuta tayari mwanaume akiwa amefariki dunia na mkewe alikuwa mahututi," alisema mtendaji huyo wa kijiji.

Alifafanua kuwa kutokana na hali aliyokuwanayo Pelepetua, wananchi waliamua kumkimbiza katika Kituo kidogo cha Afya kilichopo kata ya Itumba kwa matibabu, lakini Mganga wa kituo hicho, Efulay Malima, aliwashauri wampeleke Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Hata hivyo, alisema walipofika hospitali, Pelepetua  alifariki dunia kabla ya kupewa matibabu.

Kaimu Mtendaji wa Kata ya Itumba, Twalib Ngahoma, aliwataka wananchi wa kata hiyo kuwa makini kwa kipindi hiki cha mvua za masika kwa kuchukua tahadhari mapema ikiwamo kutokaa karibu na nyumba zenye nyufa ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na miti iliyopo karibu na nyumba zao.

Aidha, mtendaji huyo alisema mbali ya vifo hivyo, pia nyumba 25 ikiwamo ya marehemu hao,  zilianguka kutokana na mvua hiyo iliyonyesha siku tatu mfululizo.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Sono Nyaga, alithibitisha kufariki dunia kwa watu hao na kuongeza kuwa vifo hivyo vilisababishwa na kuangukiwa na kuta za nyumba waliyokuwa wakiishi.


HALI YA HEWA WATOA TAHADHARI
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), ilisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa ni za kawaida na zitaendelea kwa siku tatu mfululizo.

Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agness Kijazi, alisema mvua za msimu wa vuli zimechelewa kwani zilipaswa kuanza Oktoba hadi Desemba, mwaka huu.

Alisema mvua zilizoanza kunyesha jana jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini, zimechelewa kutokana na Pwani ya Somalia kuwa na ongezeko la joto na upepo usio na unyevu nyevu kuvuma kuelekea ukanda wa Tanzania, hivyo kuwa na joto badala ya mvua huku kukiwa na mkandamizo mdogo wa hewa kwa upande wa Msumbiji.

“Ni hali ya kawaida ndani ya msimu wa mvua kuwa na uwezekano wa mvua kubwa…mvua hii itaendelea kwa siku ya kesho (leo) na Desemba 31, mwaka huu, ikipungua au kuongezeka kwa kiwango tofauti,” alisema.

Aidha, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuwa uwezekano wa mvua kuwa kubwa upo, na kwamba inaweza kuleta madhara.

Dk. Kijazi pia aliwataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusu utabiri wa hali ya hewa wa kila siku

Grace mboka akiwa kwenye kutano wa hadhara kapunga mbarali


















Mtiania ya ubunge wa jimbo la mbarali aliyevaa kombati na skafuakiwa kwenye mkutano katika kijiji cha kapunga 
Upande wake wa kulia ni F.B.I wa chadema Bw. Allan Bujo anaye fuata  ni kamanda Vicky
Yote ni katika harakati za ukombozi wa jimbo na nchi

Monday, December 29, 2014

‘Operesheni Delete’ wabunge waliotetea Escrow bungeni yaiva


Wanasiasa wanaotajwa kuwa katika wakati mgumu wa kukubwa na kimbunga cha Escrow ni baadhi ya wabunge na mawaziri walioonekana waziwazi ndani ya Bunge kuunga mkono na kutetea uchotwaji huo haramu.
Duru za siasa zinaeleza kuwa tayari utaratibu wa kuwatambua wabunge wote waliounga mkono uchotaji huo imeanza miongoni mwa wanasiasa wenyewe.
Jambo hilo linaelezwa kufanywa pia na kambi ya upinzani Ukawa, ili kuanza mkakati maalumu utakaojulikana kama ‘Operation Delete Wabunge na Mawaziri Escrow’ itakayofanyika kwenye majimbo yote ya wabunge hao.
Hatua hiyo imeelezwa pia kuungwa mkono na wabunge wengine wa CCM waliosimama kidete kupinga na kukemea wizi huo hadi kupatikana  ushindi ndani ya Bunge lililomalizika hivi karibuni.
Wanaotajwa kuathirika zaidi ni mawaziri waliojifanya kuwatetea kwa nguvu watuhumiwa huku wakijaribu kupiga kila jambo hata lile lililoonekana kuwa lina ukweli kutoka kwenye Ripoti ya  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali.
Katika kundi la wabunge waliopona kimbunga hicho wametajwa Stephen Wasira (Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Utaribu), Profesa Mark Mwandosya (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) na  Mwigulu Nchemba (Naibu Waziri wa Fedha) ambao wanaungwa mkono hata na wapinzani kutoka na kuongoza mkakati wa kukemea mawaziri wenzao ndani ya CCM waliotuhumiwa kuchota pesa hizo.
Mawaziri wengi waliobaki wote wapo kwenye joto la kusimamiwa kidete  kuhakikisha wanang’olewa kwenye nafasi za ubunge majimboni kwao, ili kuwa funzo la kujali na kutambua maslahi ya taifa badala ya kutetea mambo na kuyachukuliwa kwa ushabiki wa vyama hata pale yanapokuwa na maslahi ya nchi.
Ni dhahiri kwamba wana CCM wa kweli wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nnauye  wamefurahishwa na uamuzi wa Bunge na kusimama hadharani kutangaza kuunga mkono maazimiom hayo ya Bunge ya kuwaweka kando mawaziri hao kutokana na kashfa hiyo iliyotikisa nchi.
CCM imepita katika wakati mgumu kutokana na kashfa hiyo, hivyo wanakijua chama hicho na wanachama wake, wanatambua umuhimu wa kuenguliwa kwa mawaziri hao kama njia mojawapo ya kukisafisha chama wakati huo wa kuelekea uchaguzi wa Serikjali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
Wanatambua kwamba kashfa ya Escrow imeacha doa kwa chama hicho na endapo hazitachukuliwa hatua kali na za wazi kuwawajibisha watendaji hao, chama  hicho kinaweza kujikuta kwenye wakati mgumu na kuadhibiwa na wananchi kwenye masanduku ya kura.
Katika kutambua hili CCM yenye hazina kubwa ya viongozi na watendaji katika kada mbalimbali inaona kwamba haiweza kupoteza lolote kuwatosa mawaziri hao  na watendaji wengine waliotajwa kwenye sakata hilo,  ili ibaki heshima  na imani  yake kwa  umma wa Watanzania.
Kuna taarifa za uhakika kwamba wananchi kwenye majimbo ya wabunge waliojifanya kusimama na kutetea uchafu  huo, hawawahitaji tena wabunge hao na tayari kuna makundi makubwa ya watu kutoka Ukawa na hata ndani ya CCM yenyewe wameanza kunyemelea majimbio hayo huku wakiungwa mkono na wananchi baada ya wabunge wa zamani kupoteza ladha kwa kutetea sukari mbovu ya Escrow.
Ni dhahiri kwamba wanaiasa hao huenda kwa kutotambua au kusoma alama za nyakati walishindwa kujipanga kuona upepo ulipoelekea. Wabunge waliosimama kupinga wizi huo, wamepanda chati ghafla na  wanatajwa kutokuwa na hofu kwenye uchaguzi mkuu ujao kwenye majimbo yao.
Inaelezwa wananchi wao wametambua kwamba wabunge hao ni wawakilishi sahihi wenye mtazamo wa kizalendo katika kutetea masuala yenye malahi ya Taifa. Wana imani nao kuendelea kuongoza majimbo hayo. Wabunge kama akina Christopher Sendeka, Kangi Lugola, Deo Filikunjombe na wengine ndani ya CCM waliovaa ujasiri na kuweka kando ushabiki wa chama kukemea wizi wa Escrow wametajwa kuwa ni wabunge wasio na wasiwasi kurudu bungeni mwaka 2015.
Waliojivika kutokuelewa na kupiga kelele kutangaza uhalali wa uovu huo ambao mwisho wa siku bunge limebaini kuwa uliokuwa  ni wizi na uchafu na kukabidhi majina ya wahusika wakuu kwa Rais Kikwete kwa hatua zaidi, sasa hivi wanatembelea kwenye kamba nyembamba.
Wabunge hao wana nafasi ndogo ya kushinda, kwani tayari wameshaonekana udhaifu wao katika kuelewa  na kutetea masuala yanayogusa taifa. Hawa wote wametajwa kuwa orodha yao itaainishwa na kupelekewa wananchi wao, ili wawakatae kwani wana upofu wa kutojua maslahi ya Taifa na ni watetezi wa watu waliopotoka.
Hivyo siku za kulia na kusaga meno kwa wabunge na wa mawaziri waliotetea Escrow ndani ya mjadala wa Bunge, zinahesabika na adhabu yao hao hakabidhiwi Rais Kikwete, bali wananchi waliowachagua.

Tusipokemea rushwa tutaiangamiza nchi yetu


TANZANIA hivi sasa inakabiliwa na rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ambayo kwa kiasi kikubwa yamechangia kusuasua kwa maendeleo.
Baaadhi ya Watanzania wenzetu wamekuwa na tabia ya kuwakejeli viongozi wanaosimama majukwaani kukemea vitendo viovu vya rushwa na ufisadi.
Tatizo la rushwa na ufisadi liliota pembe ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), hususani pale ilipojitokea kashfa ya Richomond na kumwondoa madarakani aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na viongozi wengine waandamizi wa Serikali wakimwemo mawaziri, Naziri Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.
Rushwa na ufisadi ni mambo makuu mawaili yanayotajwa na Watanzania wengi kwamba yataiangusha CCM. Viongozi wengi wa CCM wamekuwa hodari wa kutaja rushwa, lakini matendo yao hayaendani na maneno yao. Hata hivyo kuna kundi lingine ndaninya CCM linaloona kuwa kutaja rushwa ni kama kuichuria mkosi CCM. Kundi hili pamoja na kujua kwamba rushwa na ufisadi upo halidiriki hata siku moja kwa ndimi zao kukemea na kutaja neno “rushwa” au “ufisadi”.
Kundi hili linaona kana kwamba kutaja neno rushwa au ufisadi ni kujidhalilisha bila kujua kwamba kufanya hivyo kwa vitendo , ndio kukijenga na kukitakia mema chama. Kumbukumbu zipo pale Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliposimama hadharani na kukemea vitendo vya rushwa na ufisadi ndani ya  chama chake.
Kilichofuata baada ya hatua hiyo ya ujasiri, ni kiongozi huyo kupingwa  na hata viongozi wa juu wa chama, wakati huo Katibu Mkuu wa CCM akiwa Luteni mstaafu , Yusuf Makamba aliyemtaka  atumie vikao vya chama kuzungumza mambo hayo.
Tatizo linaloathiri CCM na huenda likahitimisha zama za uongozi wake ni woga wa viongozi wake kukikosoa chama na kutamka ukweli hadharani kama alivyokuwa akifanya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Kuna viongozi wachache sana ndani ya CCM wenye uwezo wa kusimama na kukosoa chama au serikalipale inapokwenda ndivyo sivyo, mfano mmojawapo wa viongozi hao, ni pamoja na Katibu Mkuu wa sasa wa CCM,  Abdulrahman Kinana.
Rushwa  iliponuka ndani ya CCM na baadhi ya viongozi wake kuonekana kero kwa umma na kuanza kukipoteze umaarufu chama hicho, kilianzisha mkakati wa kujivua gamba. Mkakati huo ulioanzishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM , Wilson Mkama ulikuwa  tiba kamili ya kuiponya CCM  na kuiepusha na viongozi wasiofaa, wala rushwa na mafisadi na hata wale wanaotajwa tajwa tu, bali kwa nia njema ya kukinusuru chama, ulikwama matokeo yake Mkama kujikuta akiwa mhanga mwenyewe kwa kuenguliwa kutoka nafasi hiyo.
Viongozi wengi wa CCM huenda ni kwa kulewa madaraka au kiburi tu, hawajitambui hususani pale wanapotembea kwenye ‘reli ya rushwa au ufisadi’. Viongozi hao wamekuwa ni mioyo migumu kama ule wa aliyekuwa mtawala wa Misri Farao, kujiuzulu kwa kosa lolote hata pale wanapohisiwa tu. Kuna hisia mbaya  ambazo wakati mwingine zinakuwa hazina ukweli, lakini kwa kiongozi madhubuti mwenye maadili ya dhati, haoni shida kujiuzulu wadhifa wake hata pale tu anapohisiwa.  Huo ndio usafi wa viongozi wenye nia na dhamira ya dhati kutumikia umma.
Tumeona  mifano ya namna viongozi wa dola nchini Kenya walivyojiuzulu akiwemo Mkuu wa Jeshi la polisi la nchi hiyo kutokana na matatizo ya kiusalama . Tukiangalia mfano huo mwema tunaoanisha na viongozi wetu hapa nyumbani  ambao hivi karibuni walizua mtafaruku mkubwa ndani ya Bunge kiasi cha kutaka kumponza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuachia nafasi yake. Viongozi hapo pamoja na mapendekezo ya kiungwana kabisa ya wabunge wa pande zote chama tawala CCM na wale wa upinzani kuwataka waachie kazi, bado wanasubiri eti mpaka  Rais awaachishe kazi!
Inasikitisha! Kwa kiongozi muungwana mtafaruku unapofikia kiwango cha juu kama ilivyotokea ndani ya mkutano wa Bunge uliomalizika hivi karibuni, hana sababu ya kusubiri eti akabidhiwe kwa mamlaka ya juu ili imwajibishe, ni wajibu wake kufanya hivyo hata kama hakufanya kosa hilo, lakini zogo pekee ndani ya Bunge linatosha kumfikisha kwenye maamuzi ya kujiuzulu, ili kulinda heshima yake na umma wa Watanzania kwa ujumla.
Kujiuzulu kwa wanasiasa ni heshima na kielelezo cha maadili mema ya utumishi wa umma, sio kusubiri utolewe ndani ya chumba wakati unaona umesabaisha ‘moshi wa kutisha’ na ili chumba kiwe salama ni wewe kutoa nje, bado unang’ang’ania.  Hapa tunapata picha na kilelezo thabiti kwamba tuna viongozi wa namna gani ambao hawawezi hata kumhurumia Rais wetu mpendwa ambaye hivi karibuni ametoka hospitali kwa matibabu makubwa.
Watu wa namna hii wanamjaribu nini Rais wetu? Rais ana watu wengi na Tanzania ina hazina kubwa ya watendaji wenye uwezo wa kutukuka na kamwe mtu mmoja hawezi kuwa bora kuliko watu wengine. Njia bora ya kiungwana ni kuchukua hatua ya kuondoka mapema kabla ya kusubiri maka Rais akuambie kufanya hivyo.
Viongozi shupavu wa kukemea rushwa kama Sumaye na wengine akina Kinana na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye,  wameuwa wakiimba juu ya tatizo la rushwa kila wakati, lakini  baadhi ya watendaji hawasikii. Mfano Sumaye karibu kila hotuba yake amekuwa akikosoa na kuonya kuhusu rushwa na ufusadi, badala ya viongozi kutuliza masikini na kutafakari hayo baadhi wanaishia hata kudhihaki maneno yake.  Kinachotia moyo ni kwamba mtu mkweli daima huwa hachoki kusema  kupigania na kusimamia kile anachoona ni kweli.
Viongozi wetu wangekuwa watu wenye kujali na kusikia maneno kama hayo naamini haya yaliyotokea ya viongozi kuchota mapesa kwa ‘lumbesa’ yasingetokea. Inasikitisha kwamba watu wa kunena na wenye maono tunao, wanaonya na kukemea lakini watu wana macho  lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, matokeo yake ni kuwa na  vongozi wa ovyo wanaoingia au kuhusishwa na mambo machafu kinyume cha maadili ya viongozi.
CCM ifike mahali sasa ikubali kukosolewa kujikosoa na kuwapa nafasi viongozi wake wanaikosoa, ili kuonyesha njia sahihi na mwelekeo wa chama badala ya kubeza wakati kuna tatizo linalotengeneza ‘kansa’ kubwa ndani ya chama.  Kama maneno ya akina Sumaye na akina Nape yasingebezwa ndani ya chama, CCM ingekuwa na viongzi waadilifu wenye miguu ya kusimama mbele ya Watanzania bila mashaka.
CCM inapokwenda kutafuta mgombea wake mwaka 2015 izingatie suala la usafi  wa kiongozi, uwezo na ujasiri wake wa kukemea, kuonya na kuonyesha mwelekeo wa maadili ndani ya chama , taifa sambamba na kujenga uchumi imara.

Dk. Slaa: Acheni kulalamika

  • Ataka Watanzania kuchukua maamuzi magumu
  • Asema dawa ni kuiondoa CCM, si kubadili viongozi
Dk. Slaa: Acheni kulalamikaKATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka Watanzania kuacha kulalamika baadala yake wachukue maamuzi magumu ya kutokichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimebobea kwa rushwa.
Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika ‘Operesheni Amsha Amsha Mzizima’, kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu.
Dk. Slaa, alisema kwamba katika kipindi cha miaka 53, CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo ya kweli na baadala yake imekuwa ikiwanyonya wanachi kutokana baadhi viongozi wake kuendekeza rushwa katika kila huduma za kijamii.
“Viongozi wote wa CCM kuanzia ngazi ya kitongoji ni wala rushwa, mfano ni pale mtu anapotaka hata kuwekewa saini kwenye barua na Mwenyekiti wa Kitongoji au Mtaa anatakiwa atoe rushwa na kwa upande wa vigogo ndio balaa,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa, aliongeza kuwa, CCM ni chama cha rushwa kwa sababu hakuna mahali popote hapa nchini mtu anaweza kupata mkopo bila kuwa na kadi ya CCM, kitendo ambacho kinawanyima baadhi ya wananchi haki.
“Tatizo la CCM sio la mtu mmoja mmoja ni tatizo la mfumo wa Chama hicho na halitaondolewa kwa kubadilisha viongozi, bali litaondoka kwa kubadilisha mfumo mzima hususani kuwachagua viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Watanzania ni walalamikaji na wanung’unikaji sana, lakini uamuzi upo mikononi mwenu… miaka 53 bado mnachagua mapanya, ukiweka chakula chako kwenye gunia la mchele hukuweka Paka, akiingia Panya anakula nusu kila gunia,” alisema Dk Slaa.
Alisema nchi haisogei mbele kutokana na watu wachache ambao ndio wanaopata kihalali huku akidai kuwa, mwaka 2007 hata Rais Kikwete alikuwepo miongoni mwa waliohusika na suala la Kampuni ya IPTL.
“CCM haina ‘shoo’ tena ya kubadilisha nchi, miaka 53 hakuna kipya kilichotokea, kuanzia sasa michango ya kipuuzi kama michango ya mwenge tunaipiga marufuku, mwenge wa Nyerere ulileta maendeleo, lakini mwenge wa Kikwete ni chanzo cha mambukizi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi,” alisema.
Naye Diwani wa Sinza, Renatus Pamba (CHADEMA), alisema mwaka 2010 wakati wanaingia madarakani, katika Manispaa ya Kinondoni walikuta mapato ya ndani yalikuwa sh bilioni 4, lakini wameweza kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha, hali iliyofanya mapato hayo kuongezeka na kufikia sh bilioni 36 hadi sasa.
Alisema hatua walizochukuwa ni kufuta mihuri yote ya wenyeviti wa serikali za mitaa na kuandaliwa ya maofisa watendaji, na walifanya hivyo kwa sababu mihuri hiyo ilikuwa ikisababisha migogoro ya ardhi.
Kwa upande wake, Maulidi Mkandu, ambaye ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia CHADEMA katika mtaa wa Mnazi Mmoja Manzese Tip top, alisema katika mtaa huo wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo uchafu, michango ya sungusungu na ujenzi wa maabara ambayo yamesababishwa na CCM kwa kuwa wabadhirifu wa fedha na kutoweka wazi mapato ya umma.
“Kama mtaniweka madarakani nitahakikisha nawafichua wabadhirifu wa fedha, hapa kuna tatizo la taka ngumu, sungusungu na maji, hatuelewi mapato yanapelekwa wapi, nawahakikishia kuwa nitafuatilia mapato na nitakuwa muadilifu,” aliwahikishia wananchi.

Utamu wa madaraka unazamisha nchi

MIAKA ya nyuma kulikuwa na kitabu kimoja cha hadithi chenye hadithi ya kusisimua ya “Muwa uliozamisha Meli” kilichoelezea Manaodha wa meli walionogewa na utamu wa muwa waliokuwa wanakula ndani ya meli kiasi cha kusahau kuongoza meli hadi ikazama.
Manahodha hawa wanafanana na viongozi wetu wa leo wanaoliongoza taifa letu na kushika nyadhifa nyeti wanaonekana kunogewa na utamu wa madaraka kiasi cha kutowajibika na kuizamisha nchi katika dimbwi la umasikini, upotevu wa rasilimali za nchi, huduma mbovu za kijamii bila kujali.
Fahari za uongozi, magari ya kifahari, posho lukuki na bahasha za bashasha zimewavua uzalendo na uwajibikaji wamebaki watupu, wameishiwa japo ni waheshimiwa.
Wamekua waking’ang’ania na kupigania, kutetea utamu wa uongozi kuliko kuwatetea wananchi na kulinda maslahi ya nchi, jambo ambalo linazidi kuizamisha meli ya Tanzania.
Ili kuendelea kufaidi utamu huu, wamewaka mifumo ya kulindana na kubebana na kutengeneza makundi ndani ya vyama vyao vya siasa, ili wabaki kuwa juu zaidi pasiwepo na kuwashusha hata kama wanaizamisha nchi.
Viongozi hawa wanafurahia na kuona fahari ya utamu wa viongozi kuliko kuwatumikia wananchi. Uongozi kwao si mzigo bali ni dili ni sehemu ya kutajirikia.
Ni wazi kuwa manahodha kama hawa wataendelea kuizamisha Tanzania yetu kama wataendelea kuachiwa uskani ilhali wako bize wanakula muwa wameshasahau uskani wao. Hawajui hata ulipo sijui wamewaachia wawekezaji, matajiri na wafanyabiashara.
Siku zote utamu ukizidi unakua sumu, Waingereza wanasema “too much of everything is harmful” utamu huu unageuka sumu na kuuwa maadili ya uongozi, uwajibikaji, usimamizi wa rasilimali za nchi unakua mbovu kwa sababu kila mtu anataka utamu.
Utamu huu wa madaraka umesababisha ulevi wa madaraka, kulewa kiasi cha kutojali wananchi ambao kibiashara ama kimtaji wanaitwa wapiga kura.
Ulevi huu ukizidi unasababisha uteja wa uongozi, kiongozi anaona kuwa hawezi kuishi bila kuwa kiongozi kwa sababu ya utamu wanataka kuwa viongozi mpaka kufa, yuko tayari kung’ang’ana kwa gharama yoyote hata kama amelisababishia taifa hasara.
Uongozi wa namna hii unafananishwa na hotcake  umesababisha watu wawe na uroho wa madaraka na uchu usiopimika hawako tayari kuukosa wanaupigania kwa gharama yoyote hata kwa rushwa, mbinu chafu, umwagaji damu, kuchakachua na aina zote za udanganyifu wanazozijua.
Utamu wa madaraka unawazidia viongozi mpaka wanasahau kuwa wameshikilia uskani wa nchi, nchi inakosa mwelekeo matokeo yake inaanza kuzama polepole.
Ulevi huu wa madaraka umesababisha athari nyingi viongozi kufanya maamuzi ambayo yanaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa mfano msamaha wa kodi kwa wawekezaji wanaovuna mabilioni ya rasilimali za watanzania na kuhodhi mamilioni ya hekari ilhali mmachinga analipa kodi licha kipato chake kidogo.
Utamu wa madaraka umewasahaulisha viongozi wengi wajibu na majukumu waliyonayo kwa nchi kiasi cha kuufanya uongozi uonekane kuwa ni ulaji ambao umekua ni dawa ya usingizi inayowafanya viongozi walale fofofo, wajisahau.
Viongozi wamelemewa na utamu wa uongozi hawataki kubeba jukumu la kujiwajibisha wala kuwawajibisha wengine kwa manufaa ya wananchi.
Kumekua na vitendo vingi vya ubadhirifu, ufisadi na wizi wa fedha za walipa kodi, lakini viongozi hawataki kuwajibika wamenogewa na utamum bora nchi izame waendelee kufaidi utamu.

Sunday, December 28, 2014

Prof. J kuwania ubunge Mikumi


Prof. Jay kuwania ubunge MikumiMKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, mwakani anatarajia kugombea Ubunge jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro.
Akizungumza na Tanzania Daima, rafiki yake wa karibu na Profesa Jay, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, alisema kwasasa yupo Mikumi kwa ajili ya kumsaidia Profesa Jay katika maandalizi ya uchaguzi mkuu hapo mwakani.
Nipo na Profesa tunawapigia kampeni wenyeviti wa mitaa na vitongoji katika uchaguzi unaoendelea, kwasababu tukiamini kwamba serikali na msingi mzuri wa uongozi inabidi uanzie chini.
Ina maana nyumba ambayo itakuwa na msingi mzuri ni nyumba bora zaidi. “Kwahiyo tupo hapa Mikumi tukijaaliwa uzima Profesa Jay mwakani ametangaza nia ya kugombea ubunge hapa nyumbani kwao.
Tumeanza kujenga mazingira kwenye uongozi wa chini ili mwakani Profesa acute kuna misingi imara na apate ubunge wa hapa Mikumi, kwahiyo yeye atagombea Mikumi na mimi nitagombea Morogoro mjini kwetu,” alisema.
Aliongeza kuwa, Mikumi ndipo kwao kabisa na Profesa Jay ambaye anatarajia kugombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), na wameamua kuingia kwenye siasa kwasababu wameshafanya sana nyimbo za kiharakati, wameshaongea mengi kupitia muziki wao lakini bahati mbaya viongozi wamekuwa na masikio magumu

Harakati

Makamanda wakiwa kwenye ofisi ya chama wilaya ya Mbarali wakiongonzwa na mwenyekiti wa chama wa wilaya PETER MWASHITI aliyevaa T-shirt nyeupe na kofia akiwa sambamba na mtia nia wa ubunge watatu kutoka kulia mwenye skafu.
Wakiwa tayari kwenda kwenye kazi za ujenzi wa chama na ukombozi wa jimbo.