Tuesday, December 30, 2014

Why Tanzanian graduates fail to impress in job interviews

Why Tanzanian graduates fail to impress in job interviews



Head of Human Resources Unit with World Food Programme, Tanzania Jamila Isdory

The current economic situation creates a sense of urgency in devising ways to boost the creation of jobs, and to improve young people’s access to those jobs. 
 
One distinct aspect of the current global labour market is that relatively high unemployment coexists with widespread recruitment challenges faced by employers.  
 
In other words, while there is currently excess labour supply in the aggregate, the distinct labour markets for specific skill sets are highly segmented and many employers are having difficulty finding individuals with the right skill sets for the business tasks at hand.  
 
It is not a secret that there is a widespread perception, right or wrong, that some Tanzanian graduates are being deliberately passed in favour of foreigners when it comes to job placements. 
 
Speaking to this paper in an exclusive interview over the weekend in Dar es Salaam, Head of Human Resources Unit with World Food Programme, Tanzania Jamila Isdory said that there are a lot of reasons that cause many Tanzanian job seekers fail in interviews.
 
Having worked in the human resources unit with different UN Agencies working in Tanzania mentioned the first reason that make many interviewees perform badly in interviews as lack of preparation.
 
To her preparation is key to having a great interview. “As a candidate you need to invest time in knowing the company and the job you are interviewing for.”
 
She further said that an interviewee should know what are the main objectives of the companies, how do they operate, where do they operate, what are the core functions for post and how does the job contribute to the company’s objectives? 
 
“By understanding these aspects, you can start preparing examples and evidences on how your skills, education, work experience, and the like are a perfect fit for the job. This will also help you to identify what you are bringing to the table and present your work more clearly and confidently,” she explained.
 
She says if job seekers will not be able to link their education, skills and experiences to the job they are applying for “it is not enough to say I have an MBA or I have five years of experience; instead you need to clarify how the MBA and the five years of experience will benefit the post and company in general.”
 
 “Failing to sell yourself – Understandably this is tricky since it is very hard to talk about yourself, but in interviews you need to put your modesty aside, many candidates make the mistake of assuming that the hiring managers have read their CVs in details, so they know their skills and potentials.”
 
She adds that hiring managers receive more than 100 applications for each post; they spend a few minutes in each CV.
Isdory says candidates need to step out of their comfort zone and use their strong points to their advantage. If you designed a new process that helped to simplify work load or wrote a proposal that won a grant, or set up a filling system that improved record keeping use it to make your case.
 
She notes that some job seekers fail to impress in job interviews because they are not solution oriented. That means they are not problem solving, but they are part of the problem.
 
She says according to her experience, when a company advertises a vacancy, one should know that it has a problem that needs to be resolved. It can be expansion of business, introduction of new services or clearing some work backlog.
 
At times this information is indicated in the advert that “We are hiring for an X position to help with implementation of this project.”
 
Isdory says “When preparing for the interview, you need to think how you can be the solution to the challenge faced by the company and come up with a few suggestions or ideas to present in the interview.”
 
Bad attitude/manner is another factor that causes job seekers to perform poorly in their interviews.
She says interviewees should avoid any bad attitudes when they are invited for an interview. 
 
According to Isdory some of these bad attitudes are such as for an interviewee to show up being late for an interview, chewing gum during the interview, keeping his cell phone on and speaking badly about previous employer. She says that is not the way to win in interviews, but it can rather deny him that post.
 
Asking wrong questions: 
She urges prospective candidates to ask work related questions, when they are given that opportunity instead of asking silly questions.
 
“This is not the time to ask about maternity leave, Hiring Managers want someone who can work on a continuous basis, since interviews are costly and time consuming; no one will hire you if they know you are thinking of taking leave soon,” she urges.
 
So in order to reach the over 800,000 Tanzanian graduates who complete their high education every year to easily secure jobs meant for them Isdory has created a website that offers free information to help job seekers, such as CV writing, and preparation for interviews; known as ww.interviewcoachtz.com

Ukiukwaji wa haki za binadamu na unyama ukatili ulipitiliza wa serikali ya ccm










2014 ni mwaka ambao ulijaa mauaji mengi ya watu wasio na hatia.
Idara ya polisi ndio inayoongza kwa kupiga na kuua watu bila sababu na polisi wamefanya hivyo kwa maagizo ya ccm.na polisi bila wao kujua wamejenga uadui mkubwa na wananchi na hii hatari kwao.
Kuna mapigano ya wakulima na wafugaji nchi nzima haya Nayo yamesababisha mauaji ya watu wengi hadi watoto.
Haya yote ukiyachunguza vizuri utakuta chama kinachoongoza nchi kimeshindwa kwa sehemu kubwa sana kusimamia 
sheria za nchi na kuongoza.
Rushwa imetawala kila kona ya nchi hadi mahakaamani ni rushwa ukweli ni kwamba ccm imeshindwa kuongoza nchi.
Watanzania lazima tuamke tutafute chama mbadala ili kuiondoa serikali ya ccm na kuweka chama kingine madarakani.

Picha juu zina onesha baadhi tu ya matuki yaliojaa umyama na ukiukwaji wa haki za binadamu ukatili wa jeshi la polisi kwa binadamu mauaji ya raia wasio na hatia mauaji ya waandishi wa habari kiukweli ni unyanyasaji uliopilizia na ukiukwaji wa haki na uhuru wa binadamu,
Matumizimabovu ya madaraka yanapelekea mauwaji na kunyanyaswaji wa rai kimsingi yote haya yanasababishwa na uroho wa madara wa serikali ya CCM
TUTAFAKARI WATANZANIA JE TUENDELEE CHINI YA SERIKALI YA CCM AU TUIONDOE HIO SERIKALI?
?

Serikali ya pata kigugumizi kusaini mkataba wa demokrasia(ACD)

Serikali inangoja nini kusaini Mkataba wa Demokrasia Afrika?




























waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro.

Serikali inahojiwa ni kipi kinachoizuia kukukubali kusaini mkataba wa Demokrasia Barani Afrika (ACD)? Pamoja na hayo inahimizwa  na  wadau wa maendeleo na utawala bora kusaini  ili kukuza kiwango cha demokrasia, uwajibikaji, utawala bora na uwazi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba (Jukata), Deus Kibamba, anasema katika mahojiano maalumu mapema wiki hii Jijini Dar es Salaam kuwa, Tanzania ni mojwapo ya nchi zinazounda  Umoja wa Afrika (AU) ambayo haijasaini mkataba huo tangu mwaka 2007.

Kutosainiwa kwa mkataba huo, anasema husababisha taifa kuendeshwa na watendaji wasiozingatia sheria, utawala bora, haki za binadamu na za walemavu, uhuru wa taarifa,  kukosekana kwa uwazi  na wajibikaji hasa nyakati za  uchaguzi.

“Tunashuhudia ongezeko la vitendo vya ufisadi vinavyoliabisha taifa hadi ngazi ya kimataifa,  baadhi ya viongozi kutumia udhaifu wa kutosainiwa kwa azimio la ACD la mwaka 2007, hivi kuna tatizo gani kutosaini?,”anahoji Kibamba .

Kwa muktadha huo, anasema serikali inatakiwa kujitathimini kupitia sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji  mwaka huu, kashfa za wizi wa fedha zilizokuwa kwenye akauti ya madeni ya nje (EPA) na tuhuma za  Richmond ili kwayo iwe funzo na msukumo wa  kuona umuhimu wa kusaini mkataba huo katika mkutano ujao wa AU.

Anasema kusimamishwa , kufutwa kazi na kuonywa kwa baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri hapa nchini ni matokeo ya ukosefu wa utendaji usiokuwa makini kutokana na kukosekana kwa shinikizo la kisheria kama vile mkataba unaotaka utiifu katika masuala mtambuka kama vile uchaguzi.

Mkataba huo pamoja na mambo mengine unazitaka nchi wanachama wa AU kuzingatia haki, uwazi, kupambana na vyanzo na viashiria vya migogoro inayoweza kutokana na uchaguzi, kuboresha taasisi zinazohamaisha uchaguzi na demokrasia.

Pia uchaguzi huru na wa haki katika nchi wanachama,uhuru wa kisheria, utawala wa kiutendaji unaochochea kukua kwa demokrasia na utawala bora pamoja na  uwazi kulingana na azimio na kanuni za AU.

Unapofika wakati wa uchaguzi, mkataba huo unaonya nchi wanachama kutoruhusu jeshi kuingilia shughuli za uchaguzi, kuwepo kwa uwazi na upatikanaji wa taarifa za uchaguzi kwa wakati ikiwamo matokeo yaliyotokana na upigaji kura.

Mambo mengine ni  kutokuwepo kwa  vitendo vya kihuni ambavyo mkataba huo unavitafsiri  kuwa ni pamoja na uchakachuaji wa kura, kuharibu uchaguzi kwa makusudi kwa masilahi ya mtu au chama chochote cha siasa na mambo mengine yanayoendana na hayo.

Kadhalka nchi wanachama wanatakiwa unapofika wakati wa uchaguzi kutambua thamani ya haki za binadamu kama vile walemavu, haki za wanawake,makundi yasiyotambulika na maalumu, kuhamasisha utawala bora na haki.

Kibamba ammbaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Taarifa kwa Umma (TCIB) anaona kama  Tanzania haijaweza kupelekea bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ya habari licha ya viongozi waandamizi kauhidi mara kwa mara kat ika mikutano ya ndani na nje ya nchi.

Anasema kwa nyakati tofauti Rais Jakaya Kikwete akiwa nchini Uingereza na Marekani, aliahidi kufikishwa bungeni kwa muswada wa habari kabala ya kumaliza kipindi chake cha uongozi, kauli ambayo amewahi kuirudia akiwa  hapa nchini pia.

“Ninaamini kwamba kupata, muswada wa habari kabla ya kumaliza muda wake mwaka 2015  ni kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano…mimi mwenyewe hivi karibuni nimeshawahi kumuuliza Spika wa Bunge Anne Makinda ikiwa huenda bunge lijalo mwezi Februari, 2015 au kabla ya Bunge la Bajeti 2015/2016 ana mpango wa kupokea muswada wa habari, lakini amenihakikishia kwamba katika orodha yake hakuna kituo kama hicho,”alidai.

Wakati Tanzania ikiendelea kusuasua kupeleka bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya  Vyombo vya Habari, Kenya wamepitisha Sheria mpya ya Usalama inayovibana vyombo hivyo na kuzua utata mkubwa na ikiwa ni pamoja na wabunge kuchapana makonde ndani ya mkutano  wa bunge.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni bunge nchini humo liligeuka `uwanja wa vita’ kutokana na baadhi ya wabunge kunyukana makonde, kuchaniana nguo na kurushiana matusi, maneno ya kebehi na kukashifiana baada ya kugawanyika kuhusu muswada huo ambao ulipitishwa kwa nguvu.

Tayari muswada huo umesainiwa na Rais Uhuru Kenyatta na sasa ni  sheria mpya ya usalama. Serikali ya Marekani  imeonyesha kutoridhishwa na namna Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usalama ulivyopitishwa nchini humo.

Kwa upande wa Tanzania imekuwa vigumu kuwa na sheria ama kanuni zinazotekelezeka za kuwabana viongozi wasiowaadilifu kwa kuwa hata ndani ya katiba pendekezwa masuala ya uadalifu kuwa tunu ya taifa yalipingwa hadharani. Hata hivyo sheria ya maadili na utumishi wa umma ni kiini macho kwa kuwa hakuna kinachoweza kumbana au kumuwajibisha kiongozi wa umma anayekiuka maadili ya utumishi.

Kiporo cha prof. Muhongo chakaribiakuchacha

Muhongo siku zahesabika wizara ya nishati na madini


Shinikizo dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, limezidi kushika kasi baada ya Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), kumuomba Rais Jakaya Kikwete, kumwajibisha ili kupisha nafasi hiyo ichukuliwe na mtumishi mwenye sifa ya kuutumikia umma.

Desemba 22, mwaka huu, Rais Kikwete alisema katika hotuba yake kwa taifa kupitia wazee wa Mkoa wa Dar es salaam kwamba amemuweka kiporo Profesa Muhongo kwa siku mbili hadi tatu kwa kuwa uchunguzi dhidi yake ulikuwa unaendelea.

Hata hivyo, tangu wakati huo, zimeshapita takriban siku tisa bila Rais Kikwete kutangaza hatima ya Profesa Muhongo kama anatimuliwa ama kubaki katika nafasi yake.

Jukata wanamuomba Rais Kikwete kuchukua hatua hiyo kutokana na Profesa Muhongo kuhusishwa katika kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Limesema hatua hiyo inapaswa kuchukuliwa na Rais Kikwete haraka dhidi ya waziri huyo kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali ya nchi kwa sasa.

Masuala hayo yanayohusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu akaunti hiyo kutokana na taarifa zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mengine yanahusu zoezi la uandikishaji wa Watanzania katika daftari la kudumu la wapigakura katika mfumo mpya wa BVR, uandikishaji wa vitambulisho vya taifa, ambayo alisisitiza yakamilike kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

Mwakagenda alisema iwapo Rais Kikwete anaona utendaji wa Profesa Muhongo unafaa, ampe kazi binafsi ya kusimamia mashamba na siyo kuutumikia umma wa Watanzania.

Hatua ya Jukata ya kutaka Profes. Muhongo kuondolewa katika wadhifa huo kwa hoja kwamba hana tena sifa za kushika nafasi hiyo ya utumishi wa umma, ni mwendelezo wa mashinikizo yanayotolewa na makundi kadhaa ya jamii kufuatia maazimio ya Bunge ya mikutano ya 16 na 17 lililoahirishwa Novemba 29, mwaka huu.

Mbali na Rais Kikwete kumfukuza kazi Profea Tibaijuka, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ameshamsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake za kuhusika na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.

Alimshauri Rais Kikwete kujipa muda wa kusikiliza ushauri wa wataalam walioko nje ya serikali, ambao watamuonyesha nia ya kutaka kunyoosha maadili ya uongozi wa kisiasa na utumishi wa umma.

“Kwa hivi sasa, wasaidizi wake wanashindwa kumshauri Rais kwa kuogopa kubanwa wao wenyewe, hivyo wameweka wigo na kuzuia ushauri huru kumfikia Rais. Na hii ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu,” alisema Mwakagenda.

Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, Mwakagenda alisema Katiba inayopendekezwa haina uhalali wala sifa.

Alisema katiba hiyo imependekezwa kwa ajili ya viongozi wachache, kwani kimeondolewa kipengele cha wananchi kuwadhibiti viongozi.

Aliongeza kuwa katiba hiyo pia ilipitishwa bila ya kuwapo kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kukosekana kwa theluthi mbili kutoka Zanzibar.

“Bunge la Katiba halikufanya vizuri na kulitokea mgawanyiko. Maridhiano hayakuwapo. Katiba hii ni mbaya. Ni ya viongozi. Haimfai mwananchi,” alisema Mwakagenda.

Kutokana na hali hiyo, alipendekeza kuahirishwa upigaji kura ya maoni ya Katiba mpya uliopangwa kufanyika Aprili, mwakani.

Badala yake, alishauri kuitishwa mkutano mkuu wa taifa kuhusu Katiba utakaoshirikisha wadau na vyama vya siasa na kutoa mwongozo wa masuala yenye utata.

“Mchakato usimamishwe, Rais ajaye ataundeleza, tayari Rais Kikwete ameshajijengea sifa na heshima kwa kuuanzisha mchakato huu. Pia Watanzania wengi hawajafahamu kilichopendekezwa, kwani bado hawajapata nakala ya Katiba na Wizara ya Katiba na Sheria imeshasema haijachapisha nakala,” alisema Mwakagenda.

MNYIKA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitawahamasisha wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuibana serikali bungeni kulieleza Bunge sababu za kushindwa kuwafungulia mashitaka ‘wapambe’ wa watu wanaotuhumiwa kuiba nyaraka za Bunge.

Nyaraka za Bunge zilizoibwa ni zile zinazohusu ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu miamala, iliyofanyika katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Tukio hilo lilitangazwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma Novemba 23, mwaka huu, ambalo katika taarifa yake, lilisema kuwa limewatia mbaroni vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka za ofisi ya Katibu wa Bunge isivyo halali.

Mbali na kuiba nyaraka hizo, vijana hao wanadaiwa kuzichakachua na kisha kusambaza mitaani ripoti ‘feki’ ya CAG.

Kauli hiyo ya Chadema ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Tanzania Bara), John Mnyika, wakati akihutubia mkutano wa hadhara juzi jioni, katika eneo la Pasua Sokoni, Manispaa ya Moshi.

Alisema kwa kuwa mamlaka ya uteuzi haijafanya uamuzi kwa ukamilifu kuhusu maazimo manane ya Bunge, Chadema itawahamasisha wabunge hao kuishinikiza serikali kueleza kwa nini inachelea kuwafikisha mahakamani wanaodaiwa kuiba nyaraka hizo.

Mnyika alisema hadi kufikia Januri 27, mwakani, kama serikali itakuwa haijawafungulia mashitaka walioiba nyaraka hizo na kuzisambaza mitaani kinyume cha sheria, atawahamasisha wabunge kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutoa maelezo inakuwaje inawalinda hadi sasa watuhumiwa hao.

“Wangapi mko tayari kupiga kura na kusimama upande wa haki? Wanyooshe vidole. Bunge linalokuja tutawahamasisha wabunge wa pande zote kuhoji ni kwa nini serikali inachelea kuwafikisha mahakamani wale walioiba nyaraka za ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha hizi,” alisema Mnyika.

Awali, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa na Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffari Michael, alimweleza Mnyika kwamba manispaa hiyo itaunda mabaraza ya maendeleo ya kata 11 kutokana na kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji.

“Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, sisi tuko vizuri katika agizo la Rais Jakaya Kikwete, kuhusu ujenzi wa maabara. Hadi sasa Manispaa ya Moshi tumefanikiwa kukamilisha maabara 40 kati ya 49,” alisema Michael.

Aliongeza: “Hii ni hatua kubwa na ambayo wenzetu wanajiuliza, inakuwaje wapinzani wanafanikiwa kuliko maeneo yanayoongozwa na chama tawala.”

Akihutubia mikutano ya hadhara iliyofanyika Shule ya Msingi Chombo kata ya Uru Kusini na Kirima Kati, Jimbo la Moshi Vijijini, Mnyika aliwataka viongozi wa Chadema kuanza operesheni maalum ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura kwa kuwa vitambulisho walivyonavyo havitatumika katika kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa pamoja na uchaguzi mkuu.

“Lazima muwaambie ukweli wananchi wa majimbo ya Siha, Moshi Vijijini, Moshi Mjini, Same Mashariki, Same Magharibi, Mwanga na Hai wajitokeze, wasiache kujiandikisha kwenye daftari la wapigakura, kwa sababu vitambulisho walivyonavyo havitatumika katika kura ya maoni wala uchaguzi mkuu ujao,” alisema Mnyika.

Mvua za jana zaonyesha udhaifu wa miundombinu dar

Mvua yaleta maafa










Mvua  zilizonyesha jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini jana, zilisababisha maafa na kizazaa kikubwa kwa wakazi huku miundombinu mbalimbali hususan ya barabara katika mitaa mbalimbali ikifinikwa maji.

Jijini Dar es Salaam, mvua hizo zilianza saa 4:30 asubuhi na kunyesha kwa nguvu kwa takriban saa mbili, hali iliyosababisha barabara katika mitaa mbalimbali ikiwamo ya Posta na maeneo ya katikati ya jiji hilo kufurika maji na kufanya magari kupita kwa shida.

Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ulibaini kuwa maeneo mengi katika ya Jiji na mabondeni, yalifurika maji na kusababisha magari mengi na pikipiki kupita kwa shida huku na waenda kwa miguu nao wakitembea kwa taabu.

Aidha, hali hiyo ilisababisha foleni kubwa za magari katika baadhi ya mitaa hasa katikati ya Jiji.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za vifo katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na mvua hizo licha ya kuwapo kwa usumbufu mkubwa kwa wakazi wake.


MUME, MKE WAFA WAKIWA BARAZANI

Wakati hayo yakitokea jijini Dar es Salaam, mkoani Tabora watu wawili, mke na mume, wakazi wa kijiji cha Lughubu kata ya Itumba wilayani Igunga, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11:00 jioni wakiwa wamekaa barazani kwenye nyumba wanayoimiliki wanandoa hao, Ernest Makala (90) na mkewe Pelepetua Petro (80).

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, mmoja wa watoto wa marehemu, Anastazia Ernest, alisema wazazi wake walikuwa wamejipumzisha nyumbani kwao, lakini  ghafla ukuta wa nyumba ulibomoka na kuwaangukia walipokuwa wamekaa.

“Ni kweli sisi watoto tumepata pigo kubwa kwani wazazi wetu wawili wamefariki dunia, mimi nilipigiwa simu na majirani wakiniambia wazazi wangu wamepondwa na ukuta wa nyumba. Nilipofika katika eneo la tukio, nilikuta baba amefariki dunia," alisema Anastazia huku akibubujikwa na machozi.

Mtendaji wa kijiji  cha Lughubu, Hussein Mohamed, alisema yeye baada ya kufika eneo hilo, alikuta wananchi wakiwa tayari wametoa kifusi cha udongo wa nyumba iliyoanguka huku mume, Ernest Makala, akiwa tayari amekwisha kufariki dunia.

“Mimi nilikuta tayari mwanaume akiwa amefariki dunia na mkewe alikuwa mahututi," alisema mtendaji huyo wa kijiji.

Alifafanua kuwa kutokana na hali aliyokuwanayo Pelepetua, wananchi waliamua kumkimbiza katika Kituo kidogo cha Afya kilichopo kata ya Itumba kwa matibabu, lakini Mganga wa kituo hicho, Efulay Malima, aliwashauri wampeleke Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Hata hivyo, alisema walipofika hospitali, Pelepetua  alifariki dunia kabla ya kupewa matibabu.

Kaimu Mtendaji wa Kata ya Itumba, Twalib Ngahoma, aliwataka wananchi wa kata hiyo kuwa makini kwa kipindi hiki cha mvua za masika kwa kuchukua tahadhari mapema ikiwamo kutokaa karibu na nyumba zenye nyufa ikiwa ni pamoja na kukaa mbali na miti iliyopo karibu na nyumba zao.

Aidha, mtendaji huyo alisema mbali ya vifo hivyo, pia nyumba 25 ikiwamo ya marehemu hao,  zilianguka kutokana na mvua hiyo iliyonyesha siku tatu mfululizo.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Sono Nyaga, alithibitisha kufariki dunia kwa watu hao na kuongeza kuwa vifo hivyo vilisababishwa na kuangukiwa na kuta za nyumba waliyokuwa wakiishi.


HALI YA HEWA WATOA TAHADHARI
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), ilisema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa ni za kawaida na zitaendelea kwa siku tatu mfululizo.

Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agness Kijazi, alisema mvua za msimu wa vuli zimechelewa kwani zilipaswa kuanza Oktoba hadi Desemba, mwaka huu.

Alisema mvua zilizoanza kunyesha jana jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini, zimechelewa kutokana na Pwani ya Somalia kuwa na ongezeko la joto na upepo usio na unyevu nyevu kuvuma kuelekea ukanda wa Tanzania, hivyo kuwa na joto badala ya mvua huku kukiwa na mkandamizo mdogo wa hewa kwa upande wa Msumbiji.

“Ni hali ya kawaida ndani ya msimu wa mvua kuwa na uwezekano wa mvua kubwa…mvua hii itaendelea kwa siku ya kesho (leo) na Desemba 31, mwaka huu, ikipungua au kuongezeka kwa kiwango tofauti,” alisema.

Aidha, aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuwa uwezekano wa mvua kuwa kubwa upo, na kwamba inaweza kuleta madhara.

Dk. Kijazi pia aliwataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusu utabiri wa hali ya hewa wa kila siku

Grace mboka akiwa kwenye kutano wa hadhara kapunga mbarali


















Mtiania ya ubunge wa jimbo la mbarali aliyevaa kombati na skafuakiwa kwenye mkutano katika kijiji cha kapunga 
Upande wake wa kulia ni F.B.I wa chadema Bw. Allan Bujo anaye fuata  ni kamanda Vicky
Yote ni katika harakati za ukombozi wa jimbo na nchi