Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi
Wanawake wataka mafanikio zaidi
WAKATI
Tanzania ikiungana na mataifa mengine duniani kusherehekea Siku ya
Wanawake, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), umeainisha changamoto
kadhaa zinazowakabiri wananwake nchini. Anaandika Sarafina Lidwino... (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari leo
katika maadhimisho ya miaka 20 ya azimio la Ulingo wa Beijing,
Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi amesema, siku hii hukutanisha
wanaharakati wote wanaotetea haki za wanawake ili kujadili mafanikio na
changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo.
Liundi amesema, pamoja na mafanikio
waliyoyapata hususani katika nyanja za kisiasa ya kuongezeka kwa
viongozi wanawake, lakini bado kuna mapungufu katika uwezeshaji katika
uongozi wao.
Amesema, mbali na kuongezeka kwa shule,
bado hazikidhi mahitaji, majengo yapo lakini waalimu ni wachache na
wengi hawana ujuzi, mabweni hakuna, umbali mrefu unaosababisha wasichana
kupata mimba.
Kwa mujibu wa Liundi, Serikali
imejitahidi kujenga vituo vya afya, lakini changamoto iliyopo ni
wahudumu hakuna wala dawa. Hivyo waathirika wakubwa ni wanawake, haswa
wakati wa kujifungua, hukosa huduma na kupoteza maisha.
Lihundi amesema, mzigo wa majukumu
unamwelemea sana mwanamke, hivyo kukosa muda wa kushiriki katika
shughuri za kimaendeleo na uchumi.
Ameongeza kuwa bado kuna maendeleo ya
vitu wakati wananchi walio wengi wanazidi kuathirika na mfumo uliopo wa
kiuchimi; mabenki yapo lakini hakuna anayepata mkopo, soko limekuwa
holela, vitu visivyokuwa na viwango vimejaa sokono, wakati bidhaa zetu
zinakosa soko.
“Sekta zisizo rasmi, ambapo wanawake
wengi ndio wapo huko haijaweza kumkomboa mwanamke na kumtoa katika duru
ya umaskini. Ajira bado ni tatizo kubwa kwa wanawake Tanzania,” amesema
Liundi.