Nyumba zilizojengwa juu ya bomba Buruguni kuvunjwa.
25th March 2015
Rais Jakaya Kikwete.
Kikwete alisema tathmini ya nyumba ziliozojengwa juu ya bomba hilo itafanyika, na wanaanchi watalipwa fidia zao.
Kadhalika, alisema bomba hilo lililosababisha mafuriko hayo litajengwa upya ili kuwezesha kupitisha maji mengi zaidi.
Kikwete pia ameagiza wilaya ya Ilala itoe msaada wa chakula kwa wakazi hao, pamoja na misaada mingine ya kibinadamu.
“Tatizo hili linashughulikiwa na litamalizika,” alisema na
kuongeza: “Tatizo lililosababisha haya yote ni kuziba kwa bomba
lililokuwa likipitisha maji ambalo limekutwa lina vyuma, vinu, mawe na
mchanga, kwa hiyo maji yote yaliyotakiwa kupita yameshindwa kupita na
kurudi kwenye makazi ya watu.
Nyumba zote zitakazobainika kujengwa juu ya bomba itabidi zipishe,
zitavunjwa na serikali itawalipa fidia, ila tunaomba mkiondoka msirudi
tena.”
Alisema serikali itazungumza na wahandisi ili kuhakikisha bomba
hilo linajengwa katika viwango ambavyo havitasababisha tatizo jingine
kama hilo huku akiwatahadharisha wakazi wa eneo hilo kuepuka kuharibu
miuondombinu na kusababisisha kutokea kwa matatizo mengine ama hayo.
“Haya yatakwisha, lakini ninawaomba msije mkafanya tena kama haya,
ninaomba bomba litakalojengwa msiliharibu tena, mkasababisha
kutokea matatizo mengine kama haya, na wale mtakaolipwa fidia msirudi
tena hapa,” alisisitiza Kikwete.
CHANZO:
NIPASHE